image
Sakramenti

Sabaa ya Sakramenti za Kanisa Katoliki

Kanisa Katoliki lina sakramenti saba takatifu ambazo zinaonekana kama njia za kimaajabu za neema ya kimungu, zilizoanzishwa na Kristo. Kila sakramenti inasherehekewa kwa ibada inayoonekana, ambayo inadhihirisha asili isiyoonekana na ya kiroho ya sakramenti hiyo. Wakati baadhi ya sakramenti zinapokelewa mara moja tu, zingine zinahitaji kushiriki kikamilifu na kuendelea ili kukuza "imani hai" ya mshereheshaji.

Jifunze zaidi kuhusu Sakramenti

Sakramenti saba zilizowekwa na Yesu Kristo

Sakramenti Ni ishara ya wazi ionekanayo, ya neema isiyoonekana, iliyofanywa na Yesu Kristo mwenyewe, itumike kutuletea au kutuongezea neema mioyoni mwetu.

Hupewa watu wazima, vijana na hata watoto wachanga kama ishara ya kwamba wamelakiwa katika uhai mpya.

Ni sakramenti anayopewa Mkristo anapokwenda kukiri kwa majuto dhambi zake.

Ni sakramenti wanayopeana wanaarusi wakiamua mustakabali wao kuwa wa pamoja maisha yote.

Hupewa mbatizwa ili awe thabiti katika imani

Ni sakramenti ya Mkristo anapokuwa mgonjwa sana.

Ni sakramenti inayofanya Mkristo ashiriki Mwili na Damu ya Kristo.

Ni sakramenti ya kumwezesha Mkristo kuwa kiongozi ndani ya Kanisa.